Tanzanian Dream

Na Zavara Mponjika aka Chief Rhymson

Nimevutiwa na hawa jamaa Tanzanian Dream, na ningepata nafasi ya kukutana nao ningewapa madini ya ziada.  Nimefurahishwa sana na namna wanavyochana, mitambao yao iko vyema. Nimependa utumiaji maridhawa wa sitiari (metaphors), nadhani jamaa yangu X akisikia ule mstari wa “Obama bin Fande” atacheka sana.

Kibwagizo kimetulia — labda ningewakumbusha ya kwamba namba ya polisi Tanzania sio “911”, hii ni ya Marekani, bali ni 112. Tena kwa wao kuitaja nayo inaweza kuvutia pia kama ile ya awali.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Utulivu kwenye sauti zao ni jambo adimu sana, ni kama watu ambao wana uzoefu fulani. Hivi ninavyoandika nimeshafanya duru kama nne hivi kuisikiliza, na naandika huku nikiwasikiliza. Zingatia kuwa huwa sina kawaida hiyo kwa nyimbo zote za nyumbani, ila kwa wachache ambao wamefanya kazi yenye kustahili kupewa heshima kama hii. Huu waraka ni dokezo tu la hamasa niliyopata mimi mwenyewe nikiwa na mamlaka na fani hii — sidhani kama tunahitilafiana hapo. Kama emcee sio mkongwe tu bali makini, na nafuatilia kinacho.

Zama hizi tuna nafasi ya kutangaza na kusambaza kazi bila kuwa tegemezi kwa vyombo vya habari. Uchambuzi huu haupo kwa nia ya kujipatia lolote mimi na wenzangu, hususan wa Kwanza Unit  — hadi leo tunachana na kujishughulisha na utamaduni wa Hip Hop kwa ujumla. Tunajenga fani ya Hip Hop pia. Kwa kukufahamisha tu, tumekuwa na desturi ya kukagua watu wanaofanya fani hii, ambayo sisi tuna ukaribu nayo kuliko wengine hasa ukizingatia tumekua nayo; watu wanachana takribani nyundo 24 sasa, n’take radhi kabla ya kunisibahi. Yoyote anayejaribu kuingia tunamwangalia na kuona analeta nini na anaienzi vipi hii fani.

Haya ngoja nirejee kwenye mada yetu sasa. Kwa upande wa mdundo naona ni sawa kwa vile wimbo umelengwa pia kwa upande wa soko. Lakini ukiniuliza kuhusu vile vinanda, nadhani vimetawala zaidi, kitu ambacho ningekifanya pengine ni kupandisha zaidi besi na kupunja vile vinanda, maana hivyo vinanda ndio muhuri wa Bongo Flava ambayo jamaa “wameiua”.  Ingekuwa vizuri kama mdundo ungekuwa mweusi zaidi, ama hata upunjwaji wa vinanda ungeitendea haki nyimbo.

Pia, nimevutiwa na utumiaji wa uovu kuelezea jambo jema. Hii ni tafsida na ni vitu adimu sana siku hizi ambapo kila mtu anadhani michano ni mahubiri yenye vina. Uchwara wengi wameitumia Hip Hop kwa namna hii, kwa kudhania ni mteremko. Mitambao ‘baba zako mule mule’, yaani matumizi ya semi za kitaa, huwa inahakikisha wana nafasi nzuri kwenye uwanja wa Hip Hop.

Hawa jamaa kwa mbali nawafananisha na kundi moja lilikuwepo kwenye WAPI ya Dodoma. Walikuwa wanajiita jina lingine, nimelisahau lakini nalo pia lilikuwa la kikoloni. Nilivutiwa sana na hao jamaa, sasa katika maongezi yetu nao, ni kuwa niliwashauri ingefaa wajiite jina tu la Kibongo maana ndio linashika sana hasa kwa soko la nje.

Kwa upande wa hawa jamaa sijui kwa kiasi gani utayari wao ulivyo, ila siwafichi, ingekuwa vizuri kama wangekamilisha mviringo mzima (nyuzi 360) wa uwakilishaji wao — jina lingehusiana na mahala wanakotoka kwa lugha ya Kiswahili au ya kwao. Hizi ni nasaha tu, wana hiari ya kufuata au la.

Makala nyingine:

Tunatumaini Zavara ataendelea kutuletea kila atakachoona kinafaa kwenye kona yake: “Jicho la Zavara“. Kama alivyofanya kwenye hii makala yake ya kwanza kwenye tovuti ya TZhiphop, atakuwa anazungumzia nyimbo zinazomgusa na kujaribu kutoa ushauri kwa wasanii chipukizi na wale wanaofahamika ila wangependa kujiendeleza. Ushauri, michango na maoni zaidi — hasa kutoka kwa wakongwe — yanakaribishwa.

Categorized Jicho La Ra and tagged , ,
Get permanent URL | Follow RSS for this post.

8 Comments

 1. Posted February 13, 2012 at 10:13 pm | Permalink

  Shukran kwa kutoa mwanga tofauti kuhusu sanaa, siasa na mitazamo ulimwengu kupitia nasaha na uchambuzi wa ndg. Zavara Mponyika. Uchambuzi wa namna hii ni adimu sana katika vyombo vya habari Tanzania, kwa hilo tunashukuru na tunasubiria kwa hamu nakala mpya ya nasaha na mitazamo yake.

 2. Posted February 13, 2012 at 10:38 pm | Permalink

  Kinanda kiko chini saana..sio kama vile vya FuLevya kabisa.. J Ryder what up!!..http://bongoboombap.blogspot.com/

 3. ak 47(bunduki)
  Posted February 14, 2012 at 7:50 am | Permalink

  kazi nzuri sana

 4. ak 47(bunduki)
  Posted February 14, 2012 at 7:54 am | Permalink

  KWANZA UNIT,ina watu ambao wanamchango mkubwa sana katika kazi zangu,kwahiyo sitii neno kwa ZAVARA na yeye tu bali wote wanao unda kundi la KWANZA UNIT.

 5. Micky
  Posted February 14, 2012 at 4:45 pm | Permalink

  Alwayz,anytym…mch lov n respect kwa bro Zavara

 6. Posted February 16, 2012 at 6:54 pm | Permalink

  Mimi nakubaliana na zavara mcees waache mahubili yenye vina

 7. Posted February 28, 2012 at 7:18 am | Permalink

  Ala na mashairi yameiva na falsafa ya kitaa, muono dunia wa kiafrika na umahiri wa lugha unaochanganya fikra za kidini, kimila, kisekula na technologia. Endelea na kazi njema tunasikilizia toka USA.

 8. Posted March 4, 2012 at 3:28 pm | Permalink

  Kazi nzuri inapaswa kuhifadhiwa kwa kila mtu mpya katika sanaa!!

What do you think?

Your email is never published nor shared.