Ukurasa wa 9 Agosti

Leo, tarehe 9 Agosti, ni siku ya kuzaliwa ya Feisal, mtoto wa yule emcee aliyezaliwa 13 Agosti — anakwambia kuna tofauti kubwa kati ya kuwa “baba mzazi” na “baba”. Baba mzazi haoni majukumu yanayoambatana na kuzaa; baba anaelewa anachopaswa kufanya; hata kama ikionekana ni kitu kidogo sana mbele ya watu — kwa mfano, kutunga wimbo kwa ajili ya kijana wake anayetimiza miezi kumi na miwili leo hii.

1. Msikilize Fid Q akitoa nasaha kwenye wimbo “Feisal“:

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Wimbo unapatikana hapa [bofya].

2. Kurasa — Silabi

Wachache wetu labda tumeshasikia jina lake mitaani. Lakini wengi hatukupata nafasi ya kupata na kusikiliza nyimbo zake kwa makini. Bahati nzuri kuna mtu amejitolea kututumia nyimbo zake kadhaa ambazo tutazifanyia kazi zaidi, ukiacha kuziweka tu hapa kama ifuatavyo…

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

3. Kurasa — Take Care

Nina uhakika wengi hamtatosheka kusikiliza wimbo mmoja tu. Kwa hiyo, tunawapa jiwe la pili.

Kama tulivyoahidi hapo juu, tutazifanyia kazi nyimbo zake. Endelea kutembelea kijiwe hiki!

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

4. Klean Heart — Pesa

Huyu kijana anatoka/anaishi Malindi (Kenya), ila ameona sio vibaya Watanzania wakisikiliza kazi yake pia. Labda midundo sio ya Hip Hop, ila sikiliza anachosema kwenye ushairi wake:

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Bofya hapa ili usikilize nyimbo tulizozitambulisha siku chache zilizopita. Nyimbo zaidi zinapatikana kwenye TZhiphop playlist.

Categorized Audio and tagged ,
Get permanent URL | Follow RSS for this post.

One Comment

  1. Posted September 7, 2011 at 12:29 pm | Permalink

    Respect

What do you think?

Your email is never published nor shared.